Mark 8:27-29

27 aIsa na wanafunzi wake wakaondoka kwenda katika vijiji vya Kaisaria-Filipi. Walipokuwa njiani, Isa akawauliza, “Watu husema mimi ni nani?”

28 bWakamjibu, “Baadhi husema wewe ni Yahya Mbatizaji, wengine husema ni Ilya, na bado wengine husema wewe ni mmojawapo wa manabii.”

29 cAkawauliza, “Je, ninyi mnasema mimi ni nani?”

Petro akajibu, “Wewe ndiwe Al-Masihi.”
Al-Masihi maana yake ni Masiya , yaani Aliyetiwa mafuta.

Copyright information for SwhKC